JENEZA LAZIKWA TUPU MWILI WASAHAULIKA NDANI
Tukio la kushangaza limetokea katika kijiji cha Ikuti, kitongoji cha Kinyika, kata ya Ikuti wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya wananchi waliokuwa wamemzika Maulid Bukuku kurejea nyumbani na kuu mwili kuta wake ukiwa bado umelazwa kitandani.
Awali, wananchi pamoja na ndugu wa marehemu walikuwa wameelekea makaburini kwa ajili ya mazishi na shughuli shughuli hiyo wakiamini wamemlaza katika nyumba yake ya milele.
Hata hivyo, waliporudi nyumbani walipatwa na taharuki kubwa baada ya kuukuta mwili wa marehemu ukiwa bado ndani ya nyumba hali iliyozua sintofahamu kubwa.
Baadhi ya wananchi walidai huenda labda amefufuka huku wengine wakisema “amegoma kuzikwa,” jambo lililosababisha taharuki na kukimbia huku na kule wakishindwa kuelewa kilichotokea.
Baada ya hali kutulia na wafiwa kutafakari kwa kina, ndipo walipobaini kuwa katika pilikapilika za maandalizi ya mazishi walipeleka jeneza makaburini bila kuweka mwili wa marehemu ndani yake, na hivyo kuuzika mwili “kwa kusahau.”
Kutokana na tukio hilo, taarifa zilitolewa kwa uongozi wa kijiji kupitia mwenyekiti wa kijiji cha Ikuti, Hakimu Njela, ambaye aliwasiliana na Jeshi la Polisi pamoja na polisi kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.
Baada ya kupata ruhusa rasmi, kaburi lilifukuliwa mbele ya wananchi na ndugu wa marehemu ambapo ilibainika kuwa jeneza lilikuwa tupu kabisa, hali iliyothibitisha kuwa mwili wa marehemu haukuwa umezikwa.
Hatimaye, mwili wa marehemu ulirejeshwa makaburini na mazishi kufanywa upya kwa kufuata taratibu zote zinazostahili.
Chanzo: Atuganile Mwakyosa
*🍃 DUKA LA JM – DUKA LA JEMYMONEY 🍃*
_Wauzaji na Watengenezaji wa Bidhaa Asilia, Zenye Ubora na Afya_
Karibu JM Store! Tunakuletea bidhaa bora zilizotengenezwa kwa viungo 100% vya asili, bila kifuniko, kwa ajili ya afya yako na ladha ya nyumbani kwako.
*✨ BIDHAA ZETU ZILIZOPO:*
1. *Jemytea Masala* – Chai ya viungo asilia inayopa mwili, inafukuza baridi na kuleta joto. Harufu na ladha yake ni tamu, kwa kila asubuhi na jioni.
2. *Ubuyu* – Poda safi ya ubuyu wa asili, tajiri kwa vitamini C. Inasaidia usagaji chakula, inapa nguvu na ladha nzuri unapochanganya na maji au vyakula vingine.
3. *JemyPilau Masala* – Viungo vya pilau vilivyotumika kwa ustadi. Fanya pilau yako iwe na harufu na ladha inayovutia kila mtu mezani.
*KWA NINI UCHAGUE JM DUKA?*
✅ *100% Natural* – Hakuna viambatanisho vya bandia
✅ *Ubora wa Kuaminika* – Tunasimamia usafi na ubora tangu siku mikononi mwako
✅ *Afya Bora, Maisha Bora* – Tunatengeneza kile kinachokujenga, si kukuharibia
💚 Tunauza kwa rejareja na jumla. nasi leo upate bidhaa safi, halisi na yenye ladha ya nyumbani!
_JM Store – Ladha Asilia, Afya Asilia._
*📍 TUNAPATIKANA:*
Ihuna – Mbeya | Mafinga – Iringa
_Mikoani tunatuma popote ulipo!_
*📞 WASILIANA NASI SASA:*
Piga simu na WhatsApp: *+255 712 820 748*
💚 Agiza leo upate bidhaa safi, halisi na yenye ladha ya nyumbani!
_JM Store – Ladha Asilia, Afya Asilia._



0 Comments